Changia – Arusha Ndondo Cup

Saidia Kuinua Vijana Kupitia Michezo

Kila siku, mamia ya vijana wenye vipaji wanakosa jukwaa la kuonesha uwezo wao. Kupitia Arusha Ndondo Cup, tunawaunganisha na fursa, tunawaepusha na vishawishi vya uhalifu na dawa za kulevya, na tunawapa matumaini mapya.

Lakini safari hii haiwezi kufanikishwa peke yetu. Tunahitaji msaada wako.

Michuano
0 +
Wadau wa Michezo
0 +
Timu shiriki
0

Our Services

Kwa Nini Mchango Wako Ni Muhimu

01.

Kuibua vipaji

Kila shilingi unayochangia inasaidia kijana mmoja zaidi kupewa nafasi ya kuonekana.

02.

Jamii salama

Michezo inapunguza uhalifu na inaunda mshikamano wa kijamii.

03.

Ajira na fursa

Mashindano huleta ajira, biashara ndogondogo na ukuaji wa utalii.

03.

Taifa lenye matumaini

Kupitia maandalizi ya vijana, tunaweka msingi thabiti wa Taifa Stars na timu za kimataifa za kesho.

FAQ

Namna Unavyoweza Kuchangia

1. Mchango wa kifedha

Unaweza kutuma moja kwa moja kupitia M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money au akaunti ya benki.

2. Vifaa vya michezo

Je, una jezi, viatu au mipira? Msaada wako unawapa vijana wetu zana sahihi.

3. Ushirikiano wa kibiashara

Wafanyabiashara na mashirika mnaweza kushirikiana nasi kama wadhamini.

4. Muda na utaalamu

Unaweza kujitolea kama kocha, mshauri au mratibu wa vijana.

Our Services

Faida za Kushirikiana Nasi

01.

Nembo au jina lako litaonekana kwenye matangazo na matamasha yetu.

Kupitia mashindano na akademi zetu, vijana wanapata nafasi ya kuonesha uwezo wao na hata kufika kwenye timu kubwa.

02.

Utatambulika kama sehemu ya taasisi inayounda kesho bora kwa vijana.

Michezo hupunguza uhalifu, dawa za kulevya na msongo wa mawazo huku ikileta mshikamano wa kijamii.

03.

Utajivunia kuona mchango wako ukibadili maisha ya vijana moja kwa moja.

Michezo huleta fursa za biashara, ajira na kuongeza wageni kwa sekta ya utalii.

Shuhuda

Ushuhuda Kutoka kwa Waliowahi Kusaidia

Mdau, Arusha

Nilipochangia vifaa vya michezo, niliona moja kwa moja vijana wakipata furaha na nafasi ya kucheza. Hii imenipa sababu ya kujivunia kila siku.

Mdhamini, Arusha

Kama kampuni, kushirikiana na Arusha Ndondo Cup kumeongeza thamani ya chapa yetu na kutuunganisha zaidi na jamii.

Popular Classes

Jiunge na Harakati Hii Leo

Msaada wako, mdogo au mkubwa, ni cheche inayowasha ndoto kubwa. Kila kijana anayepata nafasi kupitia Arusha Ndondo Cup ni ushindi kwa taifa zima.