Arusha Ndondo Cup ni taasisi ya michezo yenye makao makuu mkoani Arusha kata ya Mlangarini mtaa wa Olomitu, inayojihusisha na kuandaa mashindano ya michezo na miradi ya vijana. Tumejikita katika kuibua vipaji, kuunganisha jamii na kukuza sekta ya michezo nchini Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki.
Kuona Tanzania yenye vijana wenye fursa, vipaji vilivyotambulika kimataifa, na jamii zilizo salama, zenye mshikamano na maendeleo endelevu kupitia michezo.
Tunaamini mshikamano kati ya vijana, jamii na wadau ndio msingi wa mafanikio.
Tunatekeleza miradi yetu kwa uwazi na kuzingatia matokeo chanya kwa jamii.
Tunaendeleza majukwaa ya kipekee ya michezo na elimu ili kuibua vipaji.
Tunathamini kila kijana, kila mchezaji na kila mdau anayeungana nasi.
Kila kijana ana ndoto, kila jamii ina matumaini, na kila taifa linahitaji mashujaa wake. Arusha Ndondo Cup iko hapa kuunganisha haya yote kupitia michezo.
Jiunge nasi kupitia WhatsApp au simu na tuandike historia mpya ya michezo Tanzania.
Ni taasisi inayoendesha michuano ya michezo na mipango ya vijana nchini. Tunawaunganisha vijana, wadau wa michezo na jamii kwa pamoja ili kuibua vipaji, kuongeza mshikamano na kukuza sekta ya michezo na utalii. Ushirikiano wetu na TFF, mashirika ya serikali na binafsi, pamoja na historia ya mashindano yaliyofanikiwa, ni ushahidi kuwa tunaweka vitendo kwenye maneno.
258 Olomitu,Mlangarini, Arusha 23218
Tunafungua kuanzia 08:00AM-05:00PM
Huwa hatufungui
Copyright © 2025 Arusha Ndondo Cup. Imetengenezwa na MattyTech Global Inc.